Sunday, 4 September 2016

SAKATA LA MBOWE NA NHC KATIKA JENGO LA CLUB BILICANAS


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amefunguka kuhusiana na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuondoa mali zake nje kwa madai ya kudaiwa kodi.

Aidha, shirika la Nyumba kupitia kampuni ya udalali juzi ilitoa samani mbalimbali katika jengo la Club Bilicanas ambalo lina ofisi ya Free Media.

Kufuatia kitendo hicho Mbowe amekanusha vikali kudaiwa fedha kwa madai kuwa amekuwa akilipa na kulitumia jengo hilo kwa takribani miongo miwili.

Mbowe amesema sababu ya yeye kutimuliwa ni siasa akidai kuwa wanafanya ili kumkomoa kwa sababu ya misimamo yake ya kisiasa hapa nchini.

Aliongeza kuwa kama kweli shirika hilo lina nia ya dhati ya kukusanya kodi, je ni watu wangapi wanadaiwa? Kama wapo wengine kwa nini hadi sasa ni samani zangu tu zimetolewa?alihoji Mbowe.

Baada ya Mbowe kuondolewa samani zake wengine wanaodaiwa na shirika hilo ni Ofisi ya Rais Milioni 10, Wizara ya uchukuzi zaidi ya Bilioni 2, Wizara ya Ujenzi inadaiwa Bilioni 2, Wizara ya Habari, Utamaduni sanaa na Michezo inadaiwa Bilioni moja.


Taasisis nyingine ni Wizara ya mambo ya nje ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa inadaiwa milioni 613 na Tume ya Haki za Binadamu Utawala Bora inayodaiwa milioni 360.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment