Sunday, 4 September 2016

POLISI WATUMIA RISASI KUWATAWANYA WAFUASI WA CUF LEO


Polisi wamepiga risasi hewani kuwatawanya wafuasi wanaodaiwa kuwa wa aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

Tukio hilo limetokea leo katika ofisi za makao makuu ya CUF Buguruni ambapo kuna mkutano na waandishi wa habari unaendelea hivi sasa.

Mkutano huo unaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Uongozi, Julius Mtatiro unalenga kujibu hotuba mbili zilizotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa nyakati tofauti Pemba na Unguja.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment