Tuesday, 13 September 2016

MTATURU AITAKA KAMPUNI YA SHANGA GOLD MINING KUWALIPA FIDIA WANANCHI


KAMPUNI ya Uchimbaji wa Madini ya dhahabu (Shanta Gold Mining Limited)  iliyopo katika kijiji cha Sambaru Kata ya Mang’onyi wilayani Ikungi, Mkoani Singida imetakiwa kuwalipa fidia wananchi 69 waliosalia ili kupisha mradi wa uchimbaji dhahabu katika eneo la mradi.

Mkuu wa wilaya hiyo, Miraji Mtaturu ametoa agizio hilo katika kikao cha pamoja baina ya wawakilishi wa kampuni hiyo, wawakilishi wa wananchi kutoka kijiji cha Mlumbi na uongozi wa kikosi kazi kilichopewa jukumu la kuhakikisha wananchi wote ambao watapitiwa na mradi huo wanalipwa fidia sambamba na kusimamia uhamishaji wa makazi.

Kapuni ya Shanta Gold Mine ltd imetakiwa kutumia siku 68 hadi Novemba mwaka huu kumaliza malipo ya watu 69 kati ya 136 ambao wanatakiwa kulipwa katika awamu ya pili ili wananchi hao waweze kupisha mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa umeshindwa kuanza kutokana na malalamiko ya malipo ya fidia kwa baadhi ya wananchi ambao tayari wamefanyiwa uthamini wa maeneo yao.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment