Wednesday, 7 September 2016

MTANZANIA ANAYEIMBA NYIMBO ZA INJILI APATA TUZO YA AMANI NCHINI KONGO

Add caption

Serikali ya Jamuhuri ya Demokrasia  ya Kongo imemtunuku cheti cha heshima ya kipekee (alozi wa Amani) mwanamuzi wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Mess Jakobo Chengula kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuhubiri amani na upendo kupitia nyimbo zake.

Chengula ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa moyo wangu hauna woga aliomshirikisha mwanadada Upendo Nkone ni mwanamuziki pekee kutoka Tanzania aliyetunikiwa cheti hicho cha heshima cha balozi wa Amani  baada ya kwenda kufanya huduma ya uimbaji katika nchi hiyo ya Kongo.

Akizungumza na wanahari jana, Chengula alisema ni heshima ya kipekee aliyoipata yeye na taifa lake la Tanzania  kwa watu wa mataifa mengine kuona mchango wa muziki wa injili  katika kuhubiri Amani ya Afrika na Dunia kwa ujumla .

Chengula alisema amepata cheti hicho kutokana na ujumbe mzuri ulioko katika nyimbo zake na matendo mema afanyao katika huduma yake.

Alisema ni furaha ya kipekee kwa nchi ya Tanzania kuonekana ni nchi inayojali misingi ya Demokrasia na haki jambo lililosababisha mataifa mengine kuona haja ya kutoa cheti hicho kwa mwanamuziki anayefanya kazi hiyo pia.

“Unajuaa pale tulienda katika huduma ya kuhubiri neno la Mungu na uimbaji  na tulikutana watu kutoka mataifa mbalimbali na mimi peke yangu ndiye niliyotokea Tanzania na pale kulikuwa na viongozi mbalimbali  na waimbaji wengi tena wakubwa kutoka mataifa makubwa  lakini hawakupata cheti hicho  lakini mimi nilipewa asee hii ni heshima ya pekee ambayo Tanzania imepata kupitia mimi kule nchini Kongo” alisema.

Akizungumzia maajabu yaliyotokea mara baada ya kuwasili nchini Kongo, Chengula alisema hajawahi kupata mapokezi makubwa kama aliyopata nchini humo.

“Kongo wamenionyesha kitu cha ajabu sana, wameonesha jinsi wanavyouheshimu muziki na hii ni faraja kwangu kwasababu mimi ni mmoja wa wanamuziki wa injili niliyefanya huduma hiyo kwa muda mrefu hapa nchini,” alisema.

Alisemabaada ya kutoa albamu yangu yake ya kwanza ya “Mungu Wangu Habadiliki” ameendeleea kufyatua vibao vya dini kwa kadri Mungu anavyomjalia.

Chengula alisema anatarajia kuzindua albamu yake mpya ya ‘Moyo Wangu Hauna Woga’ inayosambazwa na Msama Promotion.

Alisema uzinduzi wa albamu hiyo utakaofanyika jijini Dar eslaam  Septemba 20, mwaka huu huku akiwataka wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumpa sapoti katika utoaji wa huduma hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment