Thursday, 8 September 2016

MTALII WA KICHINA AFARIKI WAKATI AKIPANDA MLIMA KILIMANJARO

watalii

Raia mmoja wa China, Zhuu Yush, 27, amefariki dunia wakati akipanba Mlima Kililmanjaro kutokana na matatizo yanayodaiwa kusababishwa na hali ya hewa iliyopo eneo la Mlimani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amesema mauti yalimkuta raia huyo wa kigeni siku ya jana majira ya saa saba mchana maeneo ya Jiwe la Kamba, Tarafa ya Kibisho Ubwe, Wilayani Moshi.


Raia huyo anadaiwa kuingia nchini Agosti 3, mwaka huu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (KIA) ambapo alikutwa na baadhi ya vitambulisho na pasipoti ya kusafiria yenye namba E43941606.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment