Wednesday, 7 September 2016

MKURUGENZI ILEJE ATOA ONYO KALI


Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi ametoa onyo kali kwa wasimamizi wa mitihani ya kumaliza elimu ya shule ya msingi kutofanya kazi kwa mazoea ili kutoruhusu mianya itakayo wafanya wanafunzi wasiokuwa na uelewa kufaulu mitihani hiyo.

Mnasi amesema hayo wakati akitoa semina ya mafunzo kwa wasimamizi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje amesema, usimamizi hafifu wa mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na uwezo kitaaluma.

“Napenda kuwatahadharisha kuwa mnaweza mkarubuniwa kuweza kuwasaidia wanafunzi wasiojiweza ili wafaulu mitihani yao, kufanya hivyo ni kukiuka kanuni na taratibu za usimamizi wa mitihani, mimi sipo tayari kuwa jipu kwa raisi Magufuli,” amesema Mnasi.

Amesema kumekuwa na baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika lakini wameonekana kufaulu mitihani hiyo, kitendo hiki kinatia mashaka kwa wasimamizi wetu nchi kwani wasimamizi hawa wanaonekana kushidwa kufanya kazi yao kwa umakini.

Aidha kabla ya uteuzi wa Raisi John Pombe Magufuli, Mnasi ambaye kitaaluma ni mwalimu aliyekuwa afisa elimu shule ya msingi manispaa ya iringa, amesema endapo itabainikiwa kuwepo kwa ufaulu wa mwanafunzi asiyejua kusoma na kuandika mtuhumiwa wa kwanza atakuwa ni msimamizi wa mtihani na hatua
za kisheria ziachukuliwa dhidi yake.

Mnasi amesema, serikali imezingatia uwezo wa kitaaluma, uadilifu na uaminifu hivyo wasimamizi hao kupewa jukumu la kusimamia mitihani hiyo muhimu ya kitaifa.


Wasimamizi wa mitihani hiyo, walimuahidi Mnasi kuwa watasimamia mitihani hiyo kwa kanuni na sheria bila kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria na taratibu hizo zilizowekwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment