Wednesday, 14 September 2016

KATA YA GANGILONGA YACHANGAMKIA MFUMO WA ANWANI NA MAKAZI


UONGOZI wa kata ya Gangilonga mjini Iringa unatarajia kukutana na wadau wake Alhamisi ijayo kujadili maendeleo ya kata hiyo na utekelezaji wa mfumo wa anwani na makazi, shughuli itakayofanyika katika ukumbi wa Lugalo sekondari.

Wakizungumza na mtandao huu leo, Diwani wa kata hiyo Dady Igogo na Afisa Mtendaji wake, Fuad Mwasposya wamesema wanataka kata yao iwe ya kwanza mjini Iringa kuanza kutekeleza mpango huo.

Kwa kupitia mpango huo, viongozi hao walisema nyumba 1,035 zilizopo katika kata hiyo na barabara tisa zitakuwa na vibao vinavyozitambulisha.

“Majina ya mitaa na barabara yamatolewa na wananchi wenyewe kupitia mikutano yao,” alisema Mwasposya.

Igogo alisema nguzo zitakazotumika kutambulisha mitaa na barabara hizo zitatumiwa pia kutangaza biashara za watu mbalimbali ili kuiongezea kata hiyo mapato.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment