Sunday, 11 September 2016

GHARAMA ZA UENDESHAJI ZAWAGHARIMU BAADHI YA WAFANYAKAZI WA FAST JET

Tokeo la picha la fast jet

KAMPUNI binafsi ya usafiri wa anga, Fast Jet imeamua kupunguza wafanyakazi ili kwenda sambamba na gharama za uendeshaji

Mrugenzi Mtendaji wa Fast Jet, John Corse ametoa taarifa inayoeleza kuwa watapunguza wafanyakazi kutokana na mabadiliko ya kimuundo na uendeshaji.

 “Wateja wamepungua, hawapandi ndege sasa. Hivyo ili kampuni ipate faida, ni lazima ipunguze baadhi ya wafanyakazi ili kuendana na gharama za uendeshaji,” anasema Corse kwenye taarifa hiyo.

 Alipoulizwa kama sababu ya kupunguza wafanyakazi inaweza kuwa inatokana na mikakati ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Corse amejibu: “Si kwa sababu ATCL inafufuliwa bali ni changamoto za kibiashara.


 Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alitangaza kuwa ndege mbili ambazo Serikali iliahidi kuzinunua zitafika nchini kati ya Septemba 19 na 25.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment