Wednesday, 14 September 2016

GAVANA ASEMA UCHUMI UNAZIDI KUIMARIKA


GAVANA wa Benki Kuu (BoT), Benno Ndulu amesema hali ya uchumi wa Taifa ni nzuri na itaendelea kuimarika zaidi mwaka huu na kufikia ukuaji wa asilimia 7.2.

Ndulu amesema kuna viashiria vingi vinavyoonyesha kwamba hali ya uchumi ni nzuri.

Viashiria hivyo ni kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme, uzalishaji na matumizi ya saruji, kuongezeka kwa uagizaji wa malighafi nje na makusanyo ya kodi.

Amesema miradi mikubwa ya uwekezaji inayotarajiwa kuanza mwaka huu pia itaongeza kasi ya kukua kwa uchumi.

Miradi hiyo ni ujenzi wa reli ya kati, upanuzi wa bandari ya Dar, ujenzi wa bomba la mafuta na upanuzi wa viwanja vya ndege.


"Miradi hiyo itatoa fursa nyingi za ajira, matumizi ya cement yatakuwa makubwa, pia utaimarisha sekta ya usafirishaji ambayo inakua kwa asilimia 7.9" amesema Ndulu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment