Wednesday, 14 September 2016

DC MUFINDI ATAKA MIFUMO YA UMEME IKAGULIWE KUDHIBITI MAJANGA YA MOTO


MKUU wa wilaya ya Mufindi, William Jamuhuri amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri mbili za wilaya yake kukagua mifumo ya umeme katika shule za msingi na sekondari katika maeneo yao ikiwa ni moja ya mikakati ya kukabiliana na majanga ya moto.

Halmashauri hizo, ya Mafinga Mji na ya Wilaya ya Mufindi kwa pamoja zina shule 43 za sekondari na 149 za msingi zenye zaidi ya wanafunzi 85,000.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya chumba kimoja cha bweni la shule ya msingi ya walemavu Makalala na bweni la wasichana la shule ya sekondari Sadani, kwa nyakati tofauti kuteketea kwa moto ambao chanzo chake kinaelezwa kuwa ni hitilafu za umeme.

Akitoa taarifa ya wilaya hiyo kwa Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama hivikaribuni, mkuu wa wilaya hiyo alisema shughuli ya ukaguzi wa shule hizo inatakiwa kukamilika haraka iwezekanavyo.

“Na zile zitakazoonekana zina miundo mbinu chakavu ya umeme, zitatakiwa kuiondoa haraka iwezekanavyo ili kuepukana na majanga ya moto ambayo chanzo chake ni hitilafu ya umeme,” alisema.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment