Sunday, 11 September 2016

ATUPWA JELA BAADA YA KUKATAA KURUDIANA NA MUME

machozi-1

Mahakama ya Mwanzo wilayani Bukoba mkoani Kagera imemtia hatiani bibi Adventina Gosbert (28) kwa kosa la kukataa amri ya mahakama iliyomtaka arudiane na mme wake.

Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo chini ya hakimu Tumaini Kiyeyeu na kumtupa dada huyo selo kwa kipindi cha miezi miwili.

Awali dada huyo aliieleza mahakama kwamba mme wake huyo wa ndoa ambae wamezaa nae watoto wawili amekuwa akimfanyia vitendo vya ajabu pindi anapo kunywa pombe na kuvuta bangi.

Alivitaja vitendo hivyo kuwa ni pamoja na kumfanyisha mapenzi bila ridhaa yake, kufanya mapenzi mbele za watu na watoto tena mchana pamoja na kupigwa kipigo cha mwizi.


Dada huyo alisema kama mahakama inataka arudiane naye basi imuamuru huyo jamaa anayejulikana kama Ninja kuachana na hivyo vitu. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment