Thursday, 11 August 2016

VYAMA VIDOGO VYAPINGA OPARESHENI UKUTA


Vyama 10 vya siasa vya Upinzani vimejitokeza na kupinga Operesheni Ukuta ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyoitishwa septemba 1,2016.

 Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Klabu ya vyama vya siasa hapa nchini Bw. Kamarade Fahmi N Dovutwa amesema kuwa vyama 10 vya siasa vimekutana na kufanya tafakuri dhidi ya hali ya kisiasa nchini hususani kufuatia tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo kufanya maandamano na mikutano tarehe 1 Septemba.

Amesema kwa uzito mkubwa wa tamko la Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutaka amani ya nchi idumishwe, hivyo basi vyama hivyo haviungi mkono maandamano hayo.


Vyama hivyo ambavyo haviungi mkono ni pamoja na SAU, AFP, DP, D­Makini, Jahazi, UMD, NRA, UPDP,ADA,­Tadea na CCK. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment