Thursday, 4 August 2016

VIGOGO WAWILI ATC WATUMBULIWA


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewasimamisha kazi vigogo wawili wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC) kwa tuhuma za kufanya ufisadi katika masuala ya uteuzi wa marubani wanaopaswa kwenda kusoma nje ya nchi.


Vigogo hao ni Mkurugenzi Mkuu wa ATC, Kapteni Johnson Mfinanga na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa ATC, Sadick Muze. Waziri Mbarawa ametumbua majipu hayo leo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi walio chini ya Wizara yake katika Bandari ya Itunge Wilaya ya Kyela na kusisitiza kuwa hataki wafanyakazi wababaishaji.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment