Tuesday, 16 August 2016

MWAKIBINGA AMVAA DK NCHIMBI UFISADI NDANI YA UVCCM

James Mwakibinga

Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mmoja wa vijana wanaounda umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM) James Mwakibinga amefunguka nakuweka bayana kuwa hajaridhishwa na taarifa ya maazimio ya ripoti ya uchunguzi yalitolewa na baraza kuu la umoja huo, hivikaribuni.

Mwakibinga amesema ripoti hiyo imeogopa kuwajadili baadhi ya viongozi wa umoja huo ambao wametajwa katika ubadhirifu wa mali za jumuiya hiyo.

Mmoja kati ya viongozi aliyeachwa kujadiliwa, kwa mujibu wa kada huyo ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la UVCCM, Dk Emanuel Nchimbi aliyemtuhumu kuhusika na sakata la uuzaji wa viwanja vya jumuiya hivyo katika eneo la Temeke, jijini Dar es Salaam.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment