Friday, 19 August 2016

MKUU WA MKOA WA MOROGORO AWATUMBUA WATATU


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe ameagiza kusimamishwa kazi mkuu wa stesheni ya reli ya Kisaki, ofisa misitu Tarafa ya Bwakila na mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kisaki kwa tuhuma za kushirikiana na wafanyabiashara kusafirisha mbao na magunia ya mkaa kinyume na utaratibu.

Dk Kebwe ametoa agizo hilo alipotembelea stesheni hiyo na kubaini uwapo wa magunia ya mkaa 340 na mbao zaidi ya 540 vyenye thamani ya Sh27 milioni 27 ambavyo havina alama kama uvunaji ulifanyika kihalali.


“Serikali haiwezi kuvumilia mambo kama haya ni lazima wahusika wote wachukuliwe hatua, naagiza wahusika wote wasimamishwe kazi,” amesema Dk Kebwe.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment