Thursday, 18 August 2016

MDEE KUTAFAKARI UBUNGE WAKE 2020


Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima James Mdee amesema kama Mungu akimpa uhai mwaka 2020 katika Uchaguzi Mkuu atajipima kama ametekeleza ahadi za wananchi kama alivyoahidi ndipo atagombea, na kama atakuwa hajafikisha asilimia 50 ataachia mtu mwingine.

“Nitaangalia kama nimefikia asilimia 50% ya utekelezaji wa ahadi za wananchi ndipo nitafanya hivyo ila nisipotekeleza nitapisha ili mtu mwingine mwenye maono zaidi ya kwangu aweze kugombea na kuongoza jimbo hilo,”amesema Mdee.

Mbunge huyo machachari amedai kuwa kwa sasa amefanikiwa kutatua baaadhi ya kero za wananchi kama maji katika baadhi ya maeneo huku barabara nazo zikiwa zimetengenezwa na kushirikiana na wananchi katika kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo ya Mwabepande, Bunju, na Kunduchi na bado kazi hiyo inaendelea.


 Wakati huohuo Mdee amedai kuwa ataendelea kufanya mikutano ya hadhara kulingana na Katiba na Sheria za nchi zinavyosema na si vinginevyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment