Sunday, 14 August 2016

MADAWATI YA BULAYA YAPOKELEWA BAADA YA KUFUTWA JINA LAKE

IMG-20160813-WA0004

Hatimaye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jimbo la Bunda, Mkoani Mara Bi. Janeti Mayanja amepokea madawati 90 yalitolewa na Mbunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Esther Bulaya baada ya Mbunge huyo kufuta jina lake katika madawati hayo.

Awali madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walikataa kupokea madawati hayo baada ya kuandikwa jina la Mbunge huyo ilhali yalikuwa yamenunuliwa na fedha za Mfuko wa Jimbo.

Mkurugenzi Mayanja amesema kuwa amepokea madawati kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo Esther Bulaya baada ya kufutwa jina lake, ambapo madawati hayo tayari yamewasilishwa katika shule tatu zilizokuwa na uhaba.

“Tulifanya kikao na Mbunge Bulaya na tukakubaliana kuwa ni vyema majina yake yakafutwa katika madawati hayo kwa vile yalinunuliwa kwa fedha za mfuko wa Jimbo, lakini endapo mbunge atapenda kutupa madawati atakayonunua kwa fedha zake binafsi na kuandika majina yake hapo tutapokea kwa vile bado kuna tunauhitaji katika jimbo letu” alisema Mkurugenzi Mayanja.


Madawati hayo 90 yamesambazwa katika shule za Nyatwali, Nyerere na Ligamba, zilizopewa madawati 30 kwa kila moja.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment