Thursday, 4 August 2016

LISSU AFIKISHWA POLISI DAR, NI BAADA YA KUKAMATWA JANA SINGIDA


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefikishwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central) jijini Dar es Salaam leo saa 7.46 mchana huku ulinzi ukiimarishwa katika maeneo yanayozunguka kituo hicho.

Mara baada ya kufikishwa kituoni hapo, watu wengine ambao wanafika hapo kwa shida nyingine wamekuwa wakihojiwa na kisha kukaguliwa kabla ya kuruhusiwa kuingia.

Lissu alikamatwa jana baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Ikungi yaliko mako makuu ya jimbo lake.

Mwanasheria mkuu huyo wa Chadema ambaye amekuwa katika misukosuko ya kisheria katika siku za hivi karibuni, amefikishwa kituoni hapo akiwa kwenye gari la polisi aina ya Land Cruiser.


Wakati akishuka kwenye gari hilo, wafuasi wa Chadema walishangilia huku wakisema ‘people’s… power’ huku naye akiwanyoshea mkono kwa ishara ya vidole viwili.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment