Thursday, 18 August 2016

KUELEKEA DODOMA, WATUMISHI OFISI YA PM WATAKIWA KUJIPANGA KISAIKOLOJIA


Waziri Kassim Majaliwa amesema safari ya kuhamia Dodoma imeiva na amewataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wajipange kisaikolojia.

Ametoa kauli hiyo leo Agosti 18, 2016 alipokutana na kuzungumza na watumishi wa ofisi yake kutoka taasisi, idara na vitengo mbalimbali waliopo Dar es Salaam.


Waziri Mkuu amewataka watumishi hao watambue kuwa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment