Sunday, 14 August 2016

JUKWAA LA WAHARIRI LAPINGA GAZETI MSETO KUFUNGIWA


Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepokea kwa mshituko taarifa za kufungiwa kwa miezi 36 gazeti la Mseto kwa kutumia kifungu cha 25(1) cha Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976.

Kwa mujibu wa taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mwenyekiti wake, Theophil Makunga TEF imesema hawakubaliani na wala hawaungi mkono utaratibu huu wa Serikali kufungia au kufuta vyombo vya Habari.

Katika maelezo ya Waziri, Nape Nnauye anasema tangu Mwaka 2012 wamekuwa wakiwaonya Mseto bila gazeti hilo kubadilika huku Mkurugenzi wa Kampuni ya Halihalisi, Saed Kubenea amekana kupata maonyo kutoka Serikalini.

“Sisi TEF tunapinga utaratibu wa Serikali kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka na Hakimu katika kesi inazohusika.

“Tunataka mchakato wa kubadili Sheria ya kuanzisha chombo cha kitaaluma cha kusimamia wanahabari na vyombo vya habari uende haraka kwa nia ya kumaliza kadhia hii.”


 Jukwaa hilo pia limevitahadharisha vyombo vya Habari katika matumizi ya nyaraka ili kuepuka kuingia katika migogoro na Serikali, Jamii au mtu mmoja mmoja

Reactions:

0 comments:

Post a Comment