Sunday, 7 August 2016

GEREZA KUU IRINGA KUBOMOLEWA


HATIMAYE serikali imesikia kilio cha wadau wa sekta ya afya mkoani Iringa baada ya kuridhia kuhamisha gereza la mkoa wa Iringa lililopo jirani na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa ili kupisha upanuzi wa miundombinu ya hospitali hiyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameuagiza uongozi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Iringa kuanza mchakato wa kuhamisha gereza hilo kuelekea eneo la Kwakilosa lenye ukumbwa wa  hekta 325.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alimwambia waziri huyo kwamba uwepo wa gereza hilo karibu na hospitali hiyo umekuwa kero kubwa kwa watu wanaopeleka wagonjwa au kuhitaji huduma hospitalini hapo.


Kasesela alisema barabara inayopita katika gereza hilo imekuwa ikifungwa wakati wote nyakati za usiku na mara kwa mara jeshi la magereza linapokuwa katika shughuli zake zinazohitaji ulinzi mkubwa kwasababu za kiusalama na hivyo kusababisha kero kwa watumiaji wake.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment