Thursday, 11 August 2016

GAZETI LA MSETO LAPIGWA KITANZI


Serikali imelifungia gazeti la Mseto kwa kipindi cha miaka mitatu (miezi 36) kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo wa kuandika na kuchapisha habari ya uongo.

Kifungo hicho kinahusisha pia gazeti hilo kutochapishwa kwa njia nyingine yeyote ile ikiwemo kwa njia ya mitandao (Online Publication).

Kwa mujibu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, Gazeti hilo linadaiwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali kwa nia ya kumchafua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wa Serikali kwa lengo la kutaka kuchonganisha wananchi na Serikali yao ya Awamu ya Tano.

Kwa mujibu wa vyombo vya uchunguzi vya Serikali, imebainika kuwa nyaraka hiyo imeghushiwa na wahariri na hata pale walipotakiwa kuleta uthibitisho walishindwa kufanya hivyo.

Pamoja na makosa mengine, hivi karibuni gazeti hilo toleo Na. 480 la tarehe 4 hadi 10 Agosti, 2016 lilichapisha na kusambaza makala na barua ya kughushi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yenye kichwa cha habari kisemacho ‘Waziri Amchafua JPM’ Amhusisha na rushwa ya uchaguzi mkuu, ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano

Reactions:

0 comments:

Post a Comment