Thursday, 18 August 2016

DC GAMBO AUKWAA UKUU WA MKOA ARUSHA


Rais, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mrisho Gambo kuwa Mkuu Mpya wa Mkoa wa Arusha kuchukua nafasi ya Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa na kuhamishiwa TAMISEMI.

Kabla ya uteuzi huo, Mrisho Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini na anatarajiwa kuapishwa siku ya kesho Ijumaa, Agosti 19, 2016 saa 3 asubuhi Ikulu, Jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment