Thursday, 11 August 2016

CHAMA CHA SIASA CHA MAADILI NA UWAJIBIKAJI CHAFUTWA


Chama Cha Maadili na Uwajibikaji (CM­Tanzania) kimefutwa kutoka katika orodha ya vyama vya siasa vyenye usajili wa muda kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya usajili..

Chama hicho kilichopata usajili Februari 4, 2016 kimefutwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mujibu wa Kifungu cha 8 (3) na (4) cha Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kinachosema kuwa chama cha siasa chenye usajili wa muda ni lazima kiwasilishe maombi ya usajili wa kudumu ndani ya siku 180 tangu tarehe ya kupata usajili wa muda vinginevyo uhai wake unakoma baada ya siku hizo 180.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment