Thursday, 21 July 2016

WATUMISHI WAPEWA SIKU 12 KUHAMIA NYUMBA ZA NHC


Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga wanaoishi jijini Tanga, wamepewa siku 12 kuhamia katika nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizojengwa katika eneo la Kasera.

Agizo hilo lilitolewa juzi na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Anjelina Mabula baada ya kukagua nyumba 40 zilizojengwa na NHC katika eneo hilo yalipo makao makuu ya halmashauri hiyo.

Mabula alilazimika kutoa agizo hilo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Yona Maki kumwambia kuwa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo wanaishi jijini humo ambako ni umbali wa kilomita 35 kutokana na ukosefu wa nyumba za kuishi.

Katika maelezo ya ujenzi wa nyumba hizo yaliyotolewa na Meneja wa NHC Mkoa wa Tanga, Isaya Mshamba, nyumba 10 kati ya hizo zina vyumba viwili na majiko ya nje, 10 zina vyumba vitatu na majiko ya nje wakati 20 zina vyumba vitatu na majiko ya ndani. Mshamba alisema NHC ipo katika hatua za mwisho za kuiuzia 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment