Thursday, 21 July 2016

WAFUNGWA MIAKA 30 KWA KULAWITI NA UNYANG'ANYI


Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Musoma mkoani Mara, imewahukumu watu watatu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kubaka, kulawiti na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu Richard Maganga alisema juzi kuwa washtakiwa hao, wakazi wa Manispaa ya Musoma na walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti, hivyo kila mmoja atatumikia kifungo hicho jela kulingana na makosa aliyokutwa nayo.


Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Yesse Temba aliwataja washtakiwa hao kuwa ni James Janet (28), Emmanuel Juma (18) na Juma Ramadhani. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment