Friday, 8 July 2016

TRA YAZIFUNGUA OFISI ZA NIMROD MKONO


Hatimaye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  imezifungua ofisi za Kampuni maarufu ya uwakili ya Mbunge wa Butiama, Nimrod Mkono, Mkono & Advocates Co. ikiwa ni siku chache baada ya kuzifungia kwa madai kuwa kampuni hiyo inadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.

Kupitia kampuni ya udalali ya Yono, TRA  ilifungua ofisi hizo mbele ya Nimrod Mkono na binti yake.

Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amekiri kufunguliwa kwa ofisi hizo na kwamba uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuwepo kwa makubaliano kati ya pande mbili na ahadi ya kufanya malipo iliyowekwa na mkono.

Hatua hiyo imefikiwa huku kukiwa na taarifa kuwa ingawa Mkono amefungiwa ofisi zake akidaiwa kodi ya shilingi bilioni 1, yeye anaidai Serikali takribani shilingi bilioni 9 kwa kazi alizofanya ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment