Tuesday, 5 July 2016

TAASISI YA MARIDHIANO YANUIA KUWAPATANISHA UKAWA NA NAIBU SPIKA

1

Taasisi ya Maridhiano inatarajia kuwasilisha ujumbe kwa Spika wa Bunge Job Ndugai kuomba kuyakutanisha makundi mawili yanayosigana bungeni ili kuleta muafaka wenye tija kwa taifa.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo inayoundwa na viongozi wa dini, Sheikh Sadick Godigodi alisema kumeguka bunge kwa baada ya kambi ya Upinzani kutangaza kuonewa na maamuzi ya Naibu Spika, Dk. Tulia Akson kunahitaji viongozi wa dini kuingilia kati ili kutafuta suluhu.

“Tunatarajia katika Bunge lijalo litakaloanza Septemba kuwasilisha ujumbe kwa Spika ili tupewe nafasi ya kutatua mgogoro huu kwa maana wabunge wote wanatakiwa kuwepo bungeni kuwakilisha matatizo ya wananchi,” alisema Sheikh Godigodi.

Kambi ya Upinzani Bungeni ilisusia vikao vya Bunge la Bajeti kwa zaidi ya siku 70 kupinga kile kilichoita kuburuzwa na Naibu Spika katika uendeshaji wa chombo hicho cha kutunga sheria.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment