Tuesday, 5 July 2016

SUMATRA YAFUNGIA MABASI 12 YA CITY BOY

9

Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) imeyafungia mabasi 12 ya kampuni ya City boy baada ya mawili kati yake kupata ajali iliyogharimu maisha ya watu 29 jana.

Msemaji wa Sumatra, David Mziray amewaambiwa wanahabari leo kuwa kuanzia leo mabasi yanayomilikiwa na kampuni hiyo hayataruhusiwa kufanya safari kwenda mkoa wowote.

“Mabasi hayo yamefungiwa kuanzia leo kwa muda usiojulikana, ukaguzi utaanza kufanyika kupitia jeshi la polisi,” Mziray alisema.

Jana mabasi mawili ya kampuni ya City Boy yaligongana katika eneo la Maweni, mkoani Singida na kusababisha vifo vya watu 29, na kuwaacha wengine wakiwa majeruhi.


Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, ACP Thomas Sodeyeka alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na kufanya mizaha barabarani kulikofanywa na madereva hao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment