Wednesday, 20 July 2016

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU VILAINISHI VINAVYOTUMIWA NA MASHOGA


SERIKALI imepiga marufuku matumizi na usambazaji wa vilainishi  kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema hatua hiyo ni kwa ajili ya udhibiti wa Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Akizungumza  Dar es Salaam jana, alisema Serikali imezuia matumizi ya vilainishi hivyo kwa sababu vinachochea kuongezeka   vitendo hivyo ambavyo ni kinyume cha sheria za nchi.

“Ni kweli Serikali imezuia vilainishi hivyo kwa sababu ya kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Katika   wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, asilimia 23 wana maambukizi ya VVU” alisema.

“Katika nchi yetu hakuna  sheria inayoruhusu uhusiano wa jinsia moja na kuendelea kusambaza vilainishi hivyo ni kama kuhalalisha vitendo hivyo… mila na desturi zetu haziruhusu uhusiano huo,” alisema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment