Tuesday, 5 July 2016

PROFESA KABUDI AULA TIB


Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo (TIB) Prof. William Lyakurwa na kumteua Prof. Palamagamba Kabudi kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Prof. Kabudi ni mwalimu wa sheria katika chuo kikuu cha Dar es salaam.
Kufuatia mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ametengua uteuzi wa Wajumbe Bodi ya Benki hiyo na kuteua wajumbe wapya watakaodumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi unaanza leo 5 Julai, 2016.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment