Wednesday, 20 July 2016

MZINDAKAYA AACHIA NGAZI NDC


MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Crisant Mzindakaya, amejiondoa katika wadhifa wake kwa kile kilichoelezwa kuomba kupumzika.

Amechukua hatua hiyo ikiwa ni miezi michache tangu Rais Dk. John Magufuli aanze kuifanyia kazi ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo NDC nayo inaguswa.

Taarifa kutoka ndani ya NDC zinasema hatua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti huyo wa bodi imesababisha  sintofamu miongoni mwa watumishi wa shirika kuhusu masuala mbalimbali.


Kwa mujibu wa habari za kuaminika kutoka katika shirika hilo, miongoni mwa mambo hayo ni  hatima ya mishahara yao ambayo hawajalipwa kwa zaidi ya miezi minne sasa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment