Tuesday, 5 July 2016

MTUHUMIWA WA MAUAJI MSIKITINI MWANZA ADAIWA KUWATOROKA POLISI

Msikiti mwanza

Mtuhumiwa mmojawapo wa mauaji ya watu watatu katika msikiti wa Rahman Ibanda, Hamis Juma(38) anadaiwa kutoroka akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.

Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Mwanza imesema, mtuhumiwa alitoroka Julai 03 majira ya 2 usiku katika maeneo ya mlima wa Kiloleli Nyasaka wilaya ya Ilemela mkoani humo wakati akiwapeleka askari wa upelelezi kuwaonyesha eneo lingine wanapojificha majambazi wenzake.

“Baada ya askari kufika kwenye eneo la tukio ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika mlima huo walianza kurusha risasi kwa askari ndipo askari walipo taharuki na kuanza kujibu mashambulizi ya risasi kwa majambazi hao,” ilieleza taarifa hiyo.

Pindi majibizano ya risasi yakiendelea, mtuhumiwa aliyekuwa chini ya ulinzi wa askari polisi alipata mwanya na kuwatoroka askari na kutokomea kusiko julikana.

Aidha katika mapigano hayo askari walifanikiwa kukamata bunduki aina ya short gun ilyokatwa mtutu na kitako iliyokuwa na risasi moja chemba iliyotupwa na majambazi hao.

Hata hivyo taarifa hiyo imesema kuwa juhudi za kutafuta mtuhumiwa huyo zinaendelea na kuhakikisha anatiwa nguvuni na jeshi la polisi.
Taarifa hii ni kwa hisani ya Hivisasa Blog


Reactions:

0 comments:

Post a Comment