Sunday, 17 July 2016

MBUNGE ATOA MSAADA WA POWER TILLER 102 KWA VIJIJI VYA JIMBO LAKE


MBUNGE wa jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya Haroun Mulla amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla trekta ndogo “Power Tiller’ 102 zenye thamani ya Sh Milioni 510 zikiwa na lita 10 za mafuta kila moja kwa ajili ya shughuli za kilimo katika vijiji 102 vya jimbo hilo.

Mbali na kutoa msaada huo wa kila kijiji lakini pia Mbunge huyo alitoa trekta kama hizo mbili kwa Gereza la Rujewa ambapo alieza kuwa zitatumika katika shughuli mbalimbli ikiwemo kilimo na pamoja na kuchotea maji kwa ajili ya wafungwa.


Akikabidhi msaada huo Mulla  alisema kuwa wilaya ya mbarali ni wilaya ya kilimo na ufugaji hivyo msaada wake umelenga kusaidia Vijiji na mitaa ili kuchochea maendeleo Vijiji na mtaa kuwa na chanzo cha mapato na pia kuchochea kilimo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment