Saturday, 30 July 2016

MBOWE AITWA KITUO CHA POLISI


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema amepata wito kutoka Jeshi la Polisi uliomtaka kufika Polisi leo Julai 30, lakini ameshindwa kufanya hivyo kutokana na kuwepo Marangu, Kilimanjaro ambapo anahudhuria mazishi ya Baba Mzazi wa Mbunge mwenzao, Devotha Minja kupitia CHADEMA.

Katika taarifa aliyoitoa, Mbowe amesema jana usiku alipata wito huo kutoka kwa Zonal Crime Officer wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Wambura lakini hakuweza kufika kwasababu ya mazishi.

 “Kesho Jumapili Julai 31, nitakuwa katika shughuli za kuaga mwili wa mfanyakazi mwenzetu na aliyekuwa Mpiga picha wa Tanzania Daima, Ndugu Joseph Senga aliyefikwa na umauti akiwa kwenye matibabu nchini India, ikiwemo mimi kusafiri Kwimba Mwanza kwa ajili ya maziko siku ya Jumatatu Agosti 1,” amesema.


Hatahivyo kiongozi huyo wa Chadema amesema anajaribu kurekebisha ratiba zake ili aweze kwenda Polisi kesho Jumapili kwani amesisitiziwa kufanya hivyo japo hajui anaitiwa nini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment