Friday, 22 July 2016

MATUKIO YA UBAKAJI YAONGEZEKA NCHINI

Paul Mikongoti

UBAKAJI umeongezeka kwa kiasi kikubwa nchini ambako katika kipindi cha Januari hadi sasa, kesi 2,859 zimekwisha kuripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwanasheria Mtafiti wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Paul Mikongoti.

Alikuwa akitoa ripoti ya matukio ya haki za binadamu kwa   nusu mwaka ambako alisema idadi hiyo ni watoto 1,491 ambao waliripotiwa kubakwa.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment