Wednesday, 20 July 2016

MAHAKAMA YAMSAKA BABU TALE


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa hati ya kukamatwa kwa Meneja wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva ,Diamond Platnumz, Hamis Tale ‘Babu Tale baada ya kutotii amri ya mahakama ya kulipa shilingi milioni 250 katika kesi ya hati miliki.

Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na Babu Tale kutotii amri ya mahakama iliyomtaka amlipe Shekhe Hamis Mbonde kiasi hicho cha fedha.


Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment