Monday, 18 July 2016

LUKUVI AMTEUA JAJI KUCHUNGUZA MGOGORO WA ARDHI WA MIAKA 27 MOROGORO


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amemteua Jaji wa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, Jacob Mwambejele kuchunguza mgogoro wa ardhi Mkoani Morogoro uliodumu kwa kipindi cha miaka 27.

Jaji Jacob atachunguza mgogoro huo unaohusisha  Kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani vya Mfuru, Mbigiri, Mandengwa, Dumila, Matongolo  na Maboiga vilivyopo Wilaya ya Kilosa Mkoani humo ili kuweza kupatiwa suluhisho la kudumu.

Uteuzi huo umefanywa leo na Waziri Lukuvi kwa kutumia mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 18 (1) cha Sheria ya Ardhi Sura ya 113.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment