Wednesday, 20 July 2016

KILOLO YATAJWA KUWA KINARA WA HALMASHAURI ZENYE MAJUNGU NCHINI


JE wajua kwamba halmashauri ya wilaya ya Kilolo ya mkoani Iringa ndio halmashauri inayoongoza kwa majungu nchini?

Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri Tamisemi, Selemani Jafo alipokuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo jana.

Ikionekana taarifa hiyo kuwa na ukweli wa dhahiri, sehemu kubwa ya watumishi hao walikuwa wakimshangilia waziri huyo wakati akiendelea kutoa taarifa hiyo iliyohashiria kuwepo na ukweli huo.

Hata hivyo haikuwekwa wazi ni akina nani wapiga majungu mashuhuri wa halmashauri hiyo, majungu ambayo Jafo alikiri kuyafahamu na ambayo mara nyingi yamekuwa yakitengenezwa na watumishi hao pindi tu halmashauri hiyo inapopata mkurugenzi mpya.

Akimuonya Mkurugenzi mpya wa halmashauri hiyo, Aloyce Kwezi kutowakumbatia wapiga majungu hao, Jafo alisema akipuuza ushauri huo atajiweka katika mazingira ya chuki na watumishi wengine, kushindwa kutekeleza majukumu ya kimaendeleo kwa wananchi na hivyo kuwa katika hatari ya kupoteza ajira yake.  


Reactions:

0 comments:

Post a Comment