Saturday, 30 July 2016

DC KILOLO AHOFIA KUSHAMBULIWA NA NYOKA OFISINI KWAKE
MKUU wa wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah amesema uchafu, nyasi ndefu na vichaka  vilivyokuwa vimezunguka ofisi yake vilimuweka katika hatari ya kushambuliwa na wadudu wakali wakiwemo nyoka.


“Wakati nikifika wilayani hapa na kuanza majukumu yangu haya mapya takribani mwezi mmoja uliopita kwa kweli sikuridhishwa na hali ya usafi wa mazingira yake,” alisema leo wakati akishiriki shughuli ya usafi inayofanywa kila mwisho wa mwezi kwa kuzingatia agizo la Rais. 

Mbali na mkuu wa wilaya, shughuli ya kusafisha mazingira ya ofisi ya mkuu wa wilaya na mengineyo wilayani humo iliwahusisha watumishi wa halmashauri na wananchi mbalimbali.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment