Friday, 8 July 2016

CRDB IRINGA ILIVYOWAPIGA MSOSI WATEJA WAKEMKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka waumini wa dini ya Kiislam waliomaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, hivikaribuni kuendelea kuhubiri amani na upendo kwa faida ya Taifa.
  
Masenza aliyasema hayo katika tukio ambalo benki ya CRDB mkoani Iringa iliamua kupata chakula cha jioni na viongozi mbalimbali wa mkoa na wateja wake  waliojumuika kwa pamoja na waumini wa dini hiyo, waliosherehekea siku kuu ya Idd ElFitri juzi.

“Jukumu la kudumisha amani na umojakatika jamii ni jambo muhimu na linapaswa kulindwa na kila mtanzania ili kuyafanya mazingira ya nchi yaendelee kuwa yenye mvuto wa kiusalama kwa watanzania na wageni wake mbalimbali toka nje ya nchi,” alisema.

Pamoja na wito wake huo kwa waumini wa dini hiyo, Masenza aliwataka wananchi kwa ujumla wao kuwa walinzi wa taifa lao kwa kutoa taarifa za watu wanaohisi wana nia yenye v iashiria vya kuvuruga amani.

“Taarifa hizo zitaviwezesha vyombo vya dola kuchunguza na hatimaye kuwabaini na kuwashughulikia wenye nia hizo ovu,” alisema na kusisitiza kwamba bila wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali na vyombo vyake vya dola upo uwezekano wa kuingia katika matatizo yanayoweza kuharibu amani iliyopo.

Alisema ushahidi unaonesha watanzania wamekuwa wakiendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo kwasababu ya kuwepo kwa mazingira yanayowapa fursa hiyo.

Alisema amani ikiachwa ichezewe, kuna hatari ya kutokea machafuko yanayoweza kuleta madhara makubwa kwa maendeleo ya nchi na watu wake wakiwemo wanawake na watoto. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa CRDB Kanda ya Iringa, Kisa Samweli alisema  benki yao iliamua kuandaa chakula hicho ili kuimarisha umoja na wateja wao..

Alisema CRDB Iringa inayofuraha kutangaza kwamba imepata mafanikio kutokana na malengo waliyojiwekea ambayo pia yamesaidia kwa kiwango kikubwa kukuza uchumi wa Taifa na watu wake.

Kisa alitoa rai kwa watanzania kutumia benki ya crdb katika kukopa kwa lengo la kuboresha shughuli zao za kilimo, biashara, ujenzi na shughuli zingine za maendeleo. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment