Sunday, 17 July 2016

BAVICHA WASISITIZA KUFANYA MKUTANO WAO DODOMA

Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.

Baraza la Vijana la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) kwa mara nyinigine tena wamekaidi agizo la Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe na kusisitiza kuwa watakwenda Dodoma na kufanya mkutano wao Julai 20 siku chache kabla ya kufanyika kwa Mkutano Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajiwa kufanyika Julai 23, mwaka huu.

Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi amedai kuwa msimamo wa vijana wa chadema bado upo palepale wa kwenda Dodoma na kwamba mkutano huo utakuwa kwa ajili ya kupigania demokrasia na kuhakikisha mkutano wa CCM haufanyiki hadi pale Serikali itakapotoa haki sawa ya kidemokrasia kwa vyama vyote nchini.

Awali BAVICHA walipanga kwenda Mjini Dodoma kwa maelfu na maelfu kwa ajili ya kuzuia Mkutano Maalum wa CCM, ambao pamoja na mambo mengine unatarajiwa kushuhudia Rais, Dkt. John Magufuli akikabidhiwa rasmi Uenyekiti wa Chama hicho Taifa.

Hatahivyo vijana wa umoja wa CCM, UVCCM walikwishatoa onyo kwa BAVICHA na kuwaasa wasitekeleze mpango wao huo kwani watakuwa tayari kupambana nao vilivyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment