Friday, 22 July 2016

BAVICHA WAPEWA MBINU ZITAKAZOISADIA CHADEMA KUINGIA IKULU 2020

Katibu Mkuu CHADEMA, Dkt. Vicent Mashinji.

Katibu Mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dkt. Vicent Mashinji amewataka vijana wa Bavicha kutokuwa wazembe wakufikiria bali kujipanga kwa ajili ya kushika dola mwaka wa uchaguzi mkuu 2020 huku akiwapatia kanuni za kushinda uchaguzi huo.

Amesema chama chao kimejipanga kushika dola hivyo wao kama vijana wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya kufanya uchaguzi na kuwatambua wanachama hai, pia kuhakikisha vijana wanashiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika nafasi mbali mbali na kushinda.


“Nataka niwape majukumu matatu ambayo mkiyafanya hayo 2020 tutashinda nakutangazwa, moja hakikisheni tunaingiza wanachama wapya na kuwahakiki walio hai, nendeni 2019 kwenye serikali za mitaa vijana mgombee na tupate viongozi ngazi ya chini viijana wasomi, na tatu kwa mwaka huu kila kijana ajue nafasi zitakozogombewa katika eneo lake hiyo itatusaidia kushinda nafasi nyingi za madiwani  kwa Tanzania bara na visiwani  na haya ndiyo majukumu makubwa ninayowapatia,”  amesema Mashinji.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment