Monday, 18 July 2016

BAADA YA DK MAGUFULI KUMKUMBUKA, MREMA AHAIDI MAKUBWA BODI YA PAROLE

MREMA

Mwenyekiti wa Bodi ya Msamaha Taifa (PAROLE), Augustine Lyatonga Mrema amewataka watanzania wapime utendaji wake ndani ya siku 100 na kuahidi kuwa atafanya kazi hiyo kwa bidii baada ya kuaminiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mrema amesema atahakikisha anafanya kazi kwa bidii na kubadilisha tabia za wahalifu katika utekelezaji wa jukumu lake jipya.

Hivi karibuni Rais, Dkt. John Magufuli alimteua Mwenyekiti huyo wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP) kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo akitimiza ahadi yake aliyompa kiongozi huyo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana, Jimboni Vunjo Mkoani Kilimanjaro ambapo alimuahidi kuwa kama atashinda  urais atampatia kazi ya kufanya na kumuita ‘Jembe’.

Katika kampeni hizo, Mrema aliwaomba wananchi wa Vunjo kumpigia kura Rais Magufuli licha ya kwamba chama chake kilisimamisha mgombea katika nafasi ya urais katika uchaguzi huo uliofanyika mwaka jana.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment