Sunday, 31 July 2016

ALIYETENGENEZA CHOPA TUNDUMA AALIKWA AFRIKA KUSINI

Wananchi wakitazama helikopta iliyotengenezwa

Raia wa kigeni (Wazungu) kutoka nchini Afrika ya Kusini wamemtembelea Mkazi wa Tunduma, Mkoani Songwe, Adam Kinyekile, 34, ambaye ametengeneza helikopta na kumpatia mwaliko maalum wa kwenda kutembelea kiwanda chao cha kutengeneza chopa hizo huko bondeni.

Mwaliko huo umekuja huku Serikali kwa kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ikipiga ‘biti’ kali sana kwa yeyote yule anayejidai kutengeneza helikopta bila kufuata utaratibu.

Hivi karibuni, Kinyekile ambaye pia ni fundi magari alitumia ubunifu wake na kuunda helikopta ambayo ilivutia wengi sana na kupelekea Kiongozi wa Mwenge, George Mbijima akiwa Tunduma kumtembelea na kuweka jiwe la msingi katika eneo ilipo helikopta hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment