Tuesday, 19 July 2016

ADAIWA KUJINYONGA BAADA YA KUAMBUKIZWA VVU


Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Imara , Samwel Alcado (39) amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya chumba chake kutokana na kile kinachodaiwa ni kugundulika kuwa ana virusi vya Ukimwi (VVU).

Mlinzi huyo ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mji wa Zamani Manispaa ya Mpanda amejinyonga kwa kutumia shati lake. Mwenyekiti wa mtaa huo, Margret John amesema tukio hilo limetokea leo majira saa kumi na moja alfajiri ndani ya chumba alichokuwa akiishi Alcado.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho akisema uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika ili kubaini ukweli halisi wa tukio hilo

Reactions:

0 comments:

Post a Comment