Friday, 3 June 2016

YUSUFU MANJI ACHUKUWA FOMU KUTETEA KITI CHAKE YANGAAliyekuwa mwenyekiti wa klabu bingwa ya Tanzania Bara, Yanga Afrika, Yusufu Manji amechukuwa fomu ili kutetea nafasi yake kwenye uchaguzi utakaofanyika baadae mwezi huu. 

Akizungumza baada ya kuchukuwa fomu hiyo kwenye makao makuu ya klabu hiyo Jangwani jijini Dar es salaam, Manji alisema anachukuwa fomu ili kugombea tena nafasi hiyo si kwa sababu anapenda madaraka bali ni kwa uchungu alionao kwa klabu hiyo kongwe nchini Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukuwa fomu, Manji alisema kuwa anashangaa kuona shirikisho la soka nchini (TFF) na baraza la michezo la taifa (BMT) wanauvalia njuga uchaguzi huo hivi sasa wakati wao kama viongozi walitaka uchaguzi huo ufanyike miaka miwili iliyopita. Alibainisha ya kuwa mwaka 2014 walizuiwa kufanya uchaguzi mpaka warekebishe katiba, mwaka jana pia walizuiwa kwa madai kuwa uchaguzi huo ungeingiliana na uchaguzu mkuu wa Tanzania wa kumchagua Raisi na Wabunge, hivyo ilisababisha wao kutofanya uchaguzi.

Mwenyekiti huyo ameenda mbali zaidi na kudai kuwa kuna baadhi ya watu ndani ya TFF na BMT wanaifanyia hujuma klabu yao hasa kutokana na uswahiba uliopo kati ya TFF na AZAM na hilo ndilo limepelekea wao mpaka hivi leo zawadi yao ya ubingwa wa kombe la shilikisho hawajapewa. Pia Manji alitoa mfano kuwa je imeona wapi Tanzania ikasimamia uchaguzi wa Uganda au chadema wakasimamia uchaguzi wa ccm,hivyo kwanini TFF wasimamie uchaguzi wa Yanga. 

Katika hatua nyingine Manji alisema anaushahidi wa sauti walizorekodiwa baadhi ya viongozi wa TFF, BMT ambao walikuwa wakipanga njama za kumkata yeye iwapo atagombea, akaenda mbali zaidi kwa kumtaka Afisa habari wa klabu kutoa taarifa hiyo Polisi naTakukuru kwa uchunguzi zaidi.

Kwa mamlaka aliyonayo kikatiba amemsmamisha kazi mwenyekiti wa matawi ya yanga Mohamed Msumi kwa kushirikiana na viongoza waTFF kutaka kuhujumu uchaguzi wa yanga na kupanga safu ya uongozi, pia wanachama wote waliochukuwa fomu za kugombea nafasi mbali mbali kuptia TFF nao amewasimamisha.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment