Wednesday, 22 June 2016

YOUNG D AKIRI KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA


Baada ya kukanusha muda mrefu kutumia madawa ya kulevya rapa Young Dee hatimaye amethibitisha tetesi za miaka mingi kuhusu utumiaji wa madawa hayo.

Young D, amekiri tuhuma hizo  leo  mbele ya wanahabari Escape One ambapo amesema  ametumia madawa hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu.

Rapa huyo amewaomba radhi watanzania kwa vitendo hivyo na kuahidi kubadilika kwa kuwa marafiki zake ndio waliompoteza na kumuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Amedai kuwa amepewa ushauri nasaha na wataalam na kwamba ameachana na matumizi hayo.


Sambamba na hilo rapa huyo amerejea rasmi kwenye uongozi wake wa zamani, Million Dollar Boyz, MDB alioachana nao mwaka jana

Reactions:

0 comments:

Post a Comment