Friday, 24 June 2016

Ulaya yapigwa na butwaa Uingereza kuondoka

Mkuu wa muungano wa Ulaya Donald Tusk amesema kuwa mataifa yaliyosalia 27 ya EU yataendelea mbele na ushirikiano        
Marine Le Pen asema Ufaransa pia inamatamanio kama ya Uingereza
Kufuatia kufaulu kwa kura ya kujiondoa kutoka kwa muungano wa ulaya viongozi wakuu wa mataifa ya muungano wa Umoja wa Ulaya wamekuwa akielezea masikitiko yao.
Wanasiasa wakuu barani Ulaya na maeneo mengine duniani wameshikwa na mshutuko mkubwa kufuatia hatua hiyo ya Uingereza.
Mkuu wa muungano wa Ulaya Donald Tusk amesema kuwa mataifa yaliyosalia 27 ya EU yataendelea mbele na ushirikiano

Aidha amesema kuwa mataifa 6 wanachama wakuu wa muungano huo wa Ulaya yatakutana jumamosi kujadili hatma ya muungano huo ambao bado sasa unatishiwa na kujiondoa kwa mataifa mengine ambayo pia yanakabiliwa na shinikizo la kujiondoa.
Wabunge wa upinzani wa Ufaransa Uholanzi na Denmark wanatishia kuitisha kura ya maoni kama iliyoitishwa huko Uingereza.

Source:http://www.bbc.com/swahili

Reactions:

0 comments:

Post a Comment