Thursday, 30 June 2016

UKAWA WATINGA BUNGENI NA MABANGO WAKIWA NDANI YA MAVAZI MEUSI
Wabunge wa Kambi ya Upinzani leo wametoka nje ya ukumbi wa Bunge wakiwa na mabango mbalimbali yenye ujumbe wa kwenda kwa Rais Dkt John Magufuli na Naibu Spika Ackson Tulia.

Kabla ya kutoka nje, wabunge hao waliokuwa wamevalia mavazi yenye rangi nyeusi walisimama ndani ya ukumbi wa bunge kwa dakika chache huku wakiwa wamenyanyua mabango yao juu.


Huu ni muendelezo wa wabunge wa upinzani kususia vikao vinavyoendeshwa na naibu spika, Dkt Tulia wakidai kuwa amekuwa akikiuka kanuni za uendeshaji wa bunge.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment